Malumbano yanazidi kutanda katika muungano wa Azimio La Umoja kufuatia matakwa mapya yaliyotolewa na washirika wa kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka.
Wakiongozwa na Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior, kundi la viongozi wa Wiper sasa wanamtaka Kalonzo awe mgombea mwenza wa kinara wa ODM Raila Odinga katika uchaguzi wa Agosti 9, mwaka huu
“Sisi wanachama wa Wiper tumepigana sana ili Kalonzo awe mgombea kiti cha urais kwa sababu 2017 tulikuwa tumekubaliana na Raila kwamba Kalonzo atakua mgombea kiti,” he stated.
“Lakini kwa sababu Kalonzo anapenda Kenya, akakubali Raila awe mgombea kiti cha urais. Sisi tumesema na tunauliza apatiwe nafasi awe naibu wa rais wa Raila Odinga.”
+ There are no comments
Add yours