Kanisa latawala machozi baada ya Gigy Money kutoa ushuhuda wake.

Estimated read time 2 min read

Kanisa latawala machozi baada ya Gigy Money kutoa ushuhuda wake,

“Mimi jina langu halisi naitwa Zawadi ila kwa sababu ya U-staa nilijibadilisha nikaitwa Gift, mimi historia yangu ya kweli nimezaliwa (Chooni), Yesu kazaliwa kwenye Boma la Ng’ombe, mama yangu amepitia wakati mgumu sana kwasababu yangu alikuwa akikosana kidogo na marafiki zake wanamwambia ( mtu mwenyewe mtoto wako umemzalia Chooni)”

“Lakini nilimwambia mama yangu kuwa naondoka, na nikirudi nyumbani wote wanaokucheka sasa hivi watakuheshimu, namuombea sana mama yangu kila siku azidi kuwa na Imani na mimi kwasababu amenipambania akiwa mwenyewe, Baba yangu sijawahi kumuona, watu wanasema wananijua lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu anayenijua na sijawahi kuruhusu mtu anijue”- Gigy Money alipopewa nafasi ya kutoa ushuhuda kanisani kwa Prophet Malisa.

“Nilipagawa na Nabii ndio maana nimekuja Kanisani”- Gigy Money

“Mimi nimeanguka sana japo siwezi kusema nilianguka wapi, na pia naweza kusema siyo kila Nabii ninaemuona naweza kwenda kwenye kanisa lake, mimi ni Gigy Money nadhani mnajua, lakini pia nina ile hali kwamba watanionaje nikienda kanisani. Nilivyomuona Prophet Malisa kwa mara ya kwanza nilichanganyikiwa nikasema eeeh mbona Nabii Handsome hivi nikasema mtu kama huyu alifaa kuwa video King kwenye nyimbo za wasanii inakuwaje anamtumikia Mungu? lazima ana kitu”

“Nikasema mbona yupo kwa Mungu na uzuri wote huu, nikasema ngoja nimsikilize, ndio maana nimekuja hapa kusikiliza kilichopo ndani ya Nabii huyu”- Gigy Money

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours