Kenya imetangaza kuidhinisha raia wa karibu nchi zote za Afrika kuingia Nchini humo bila visa isipokuwa Somalia na Libya ambazo hazijajumuishwa kwenye mpango huo kwa sababu za kiusalama ambapo raia wa Nchi zilizopata msamaha huo wataruhusiwa kukaa Nchini humo kwa miezi isiyozidi miwili.
Kwa mujibu wa taarifa ya baraza la mawaziri Nchini humo hitaji la Uidhinishaji wa Kielektroniki wa Kusafiri, ETA, litafutwa kwa nchi zote za Kiafrika, isipokuwa Nchi hizo mbili huku wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Uganda, Tanzania, Rwanda, na Burundi) wakiruhusiwa kukaa hadi miezi sita.
Hatua ambayo inalenga kuunga mkono ukuaji wa utalii na kukuza ushirikiano wa kikanda na kurahisisha usafiri katika bara zima pia inasukumwa na Umoja wa Afrika (AU)
Mpango huu unaiongeza Kenya kwenye orodha ya nchi za Afrika ambazo zimeruhusu kusafiri bila visa, kama vile Ghana, Rwanda, Senegal, Uganda, Shelisheli, Benin, Gambia.
+ There are no comments
Add yours