Shirikisho la Soka la Libya limeamriwa kulipa faini ya TZS milioni 136.3 baada ya kuwatendea visivyo timu ya taifa ya Nigeria (Super Eagles) walipowasili nchini humo kwa ajili ya mechi ya kuwania kufuzu AFCON 2025.
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limesema mchezo huo umefutwa, na timu ya Nigeria imepewa pointi zote tatu pamoja na mabao matatu.
Nigeria ilisusia mechi hiyo baada ya kukwama uwanja wa ndege kwa zaidi ya saa 15 huku ikiilaumu Shirikisho la Soka la Libya kwa kutotuma magari ya kuwachukua hadi hotelini, ambapo ni umbali wa takriban saa 3.
+ There are no comments
Add yours