Klabu ya Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns, imetwaa ubingwa wa kombe la Afrika ‘AFL’ kufuatia ushindi wa jumla wa 3-2 dhidi ya klabu ya Wydad Casablanca kwenye fainali ya Mkondo wa pili leo Novemba 12
Fainali ya kwanza iliishuhudia Wydad ikishinda 2-1 nyumbani Mohamed V, Morocco kabla ya Sundowns kushinda 2-0 wakiwa nyumbani Loftus Versfeld, Pretoria Afrika na kuandika historia kuwa klabu ya kwanza kutwaa kombe jipya la African Football League.
Kwa kujihakikishia Ubingwa Klabu ya Mamelodi itajinyakulia kitita cha Dola za Kimarekani Milioni 4 kama zawadi.
+ There are no comments
Add yours