Donald Trump amemshinda kiti cha uraisi katika uchaguzi wa urais wa 2024 Marekani, hatua ambayo inampa muhula wa pili na kubadili rekodi iliyowekwa na Grover Cleveland, rais wa 22 na 24 wa marekani, ambaye alikuuwa rais wa kwanza aliyehudumu kwa vipindi viwili visivyo vya mfululizo.
Trump alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2016 kwa kauli mbiu ya “Make America Great Again” akimshinda Hillary Clinton. Lakini alishindwa mwaka 2020 na Joe Biden wakati wa janga la COVID-19. Safari hii, amerejea madarakani akiwa na ahadi ya “Make America Great Once Again.”
Kampeni ya #DonaldTrump iliangazia zaidi changamoto za kiuchumi, usalama wa mipaka, na mfumuko wa bei, huku akionya juu ya matokeo ya sera za Biden-Harris. Trump alikabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo jaribio la mauaji mara mbili wakati wa kampeni. Hata hivyo, aliendelea na kampeni kwa nguvu zaidi, akiungwa mkono na wafanya biashara wakubwa na baadhi ya wanasiasa wa zamani wa chama cha Democrat kama Robert F. Kennedy Jr.
#KamalaHarris aliingia kwenye kinyang’anyiro cha urais baada ya Biden kujiondoa. Kamara Harris alionya juu ya athari ya sera za Trump, hasa kuhusu haki za wanawake. Hata hivyo, ujumbe wa mwisho wa kampeni wa Trump ulisema: “Harris ameharibu, Trump atafanya marekebisho.”
Trump amekuwa na changamoto nyingi za kisheria, lakini aliendelea kutumia kesi hizo kama nguvu kwenye kampeni yake, akisema kuwa “vita vya kisheria” vilivyopangwa dhidi yake vilimpa nguvu zaidi kwenye kinyang’anyiro hicho.
Hivyo, uchaguzi wa 2024 umeleta historia mpya, na Trump ameahidi kuendelea na ajenda zake mara baada ya kuapishwa kwa muhula wa pili
+ There are no comments
Add yours