Masaibu ya Pepe Man City Yaendelea

Estimated read time 1 min read

BINGWA mtetezi wa Ligi Kuu ya Kandanda Uingereza (Epl) Manchester City wamejikuta katika hali ambayo hawajazoea miaka ya hivi karibuni.

Mechi ya Jumanne ya Kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (Ucl) dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi, iliendelea kuharibu historia nzuri ya The Citizens.

Manchester City walikuwa kifua mbele 3 – 0 ndani ya dakika 53 ya mechi hiyo. Na kipenga cha mwisho kilipopulizwa, mechi iliisha sare ya 3 – 3.

Matokeo ya mechi hii imewapa City rekodi mbaya zaidi katika mkanyagano wa mechi za klabu bingwa ulaya.

Ni timu ya hivi punde zaidi kuwahi kuacha ushindi wa mabao matatu nunge uwaponyoke katika historia ya Ligi ya Mabingwa.

Hakuna timu iliyowahi kuongoza 3-0, zikiwa zimesalia chini ya dakika 20, na kushindwa kuibuka mshindi katika Ucl.

Utepetevu wa Man City chini ya Kocha Pep Guardiola umekithiri katika mechi sita zilizopita.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours