Matiang’i Atangaza Likizo Kakamega, Mombasa na Maeneo Mengine Yatakayo Kuwa na Uchaguzi

Estimated read time 1 min read

Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i ametangaza siku ya Jumatatu, Agosti 29 kuwa sikukuu ya kitaifa katika maeneo ambayo uchaguzi unatazamiwa kufanywa.

Hii ni pamoja na kaunti za Mombasa na Kakamega ambapo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) itaendesha uchaguzi wa ugavana.

Maeneo mengine ni pamoja na; Kitui Vijijini, Kacheliba, Pokot Kusini, maeneo bunge ya Rongai na Wadi ya Kwa Njenga huko Embakasi Kusini, na Wadi ya Nyaki Magharibi huko Imenti Kaskazini.

“Waajiri kote nchini wanaombwa kuwaachilia wafanyikazi wao ambao wamesajiliwa kama wapiga kura katika maeneo yaliyoorodheshwa ya uchaguzi ili kuwawezesha kupiga kura,” Matiang’i alisema.

Tangazo hili linafuatia baada ya timu ya Uchaguzi kuhairisha uchaguzi sehemu hizo katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 9 Agosti

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours