Mbunge wa Nyali Mohammed Ali almaarufu Jicho Pevu aongoza maandamano aandamano jijini Nairobi na Mombasa kupinga uamuzi wa Mahakama ya Juu kuruhusu usajili wa vyama vya LGBTQ nchini Kenya. Maandamano hayo yalianza katika miji wa Mombasa na Nairobi baada ya sala ya Jumaa adhuhuri. Waumini wa Kikristo wakijiunga baadaye.
Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na Majaji Smokin Wanjala na Njoki Ndung’u walitoa uamuzi kwa upande wa wengi wa suala hilo, wakisema kuwa LGBTQ ina haki ya kujumuika na aina yoyote inayozuia haki yao ya ushirika ni ubaguzi. Hata hivyo, Majaji Mohammed Ibrahim na William Ouko walikataa, na kuongeza kuwa kuruhusu usajili wa shirika kama hilo ni sawa na kupigania vitendo kinyume na sheria.
+ There are no comments
Add yours