Mbunge wa Taveta, Daktari Naomi Shabani akutana na wakazi wa Nairobi kuwarai kumpa kura mwezi wa Agosti

Estimated read time 1 min read

Mbunge wa Taveta, Dr Naomi Shaban, alikutana na wapiga kura wa Taveta wanaoishi Nairobi siku ya Jumapili, tarehe 30, katika harakati zake za kuwarai wampe kura kwenye uchanguzi wa Agosti 9.

Dr. Naomi anatafuta kuungwa mkono kwa mara ya nne akiwania kiti cha ubunge Taveta kupitia tikiti ya chama cha Jubilee.

Wakazi wa Taveta wakihudhuria mkutano wa siasa wa mh. Naomi Shabani

Naomi anapokea upinzani mkali kutoka kwa washindani wake ukiongozwa na wakili Bwire wa chama cha wiper, ambaye ameonyesha nia ya kumbandua katika kiti hicho.

Wengine atakao shindana nao ni Dida Mzirai wa UDA, na Moris Mutiso wa ODM

PICHA/MH. NAOMI SHABANI AKIHUTUBIA MKUTANO WA WAKAZI WA TAVETA, MOMBASA
Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours