Mchekeshaji wa Tanzania Aliyetamba Kenya Kwa Msemo Wa ‘Kata Simu Tupo Site’ Afariki Dunia

Estimated read time 1 min read

Msanii mkongwe wa vichekesho nchini Tanzania Umar Iahbedi Issa, almaarufu Mzee Mjegeje, ambaye anatambulika mitandaoni nchini Kenya kwa kauli mbiu yake ya ‘Kata simu tupo site’ amefariki dunia.

Mzee Mjegeje inasemekana alikata roho Jumatano, Machi 20, katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, Tanzania, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Meneja wake, Real Jimmy, alithibitisha habari hizo za kusikitisha japokuwa hakufichua ugonjwa uliosababisha kifo chake.

Mwaka wa 2022, alidondosha kauli mbiu iliyovuma katika ukanda wa Afrika Mashariki, hasa nchini Kenya Kenya “Kata simu.. kata simu.. tupo site”. Kauli hiyo ilipenyeza lugha ya mtaani wa Kenya na hata kutumika kwa mijadala ya kisiasa na mienendo ya mitandao ya kijamii.

Katika kipande hicho, Megeje alinaswa kwa mbwembwe akimtaka mpigaji kukata simu. Ilionyesha akiwa amevalia mavazi ya Waislamu katika eneo la nje, ikiwa ni pamoja na skafu ya Arafat na kanzu. Kisha akaitoa simu yake iliyokuwa ikiita mfukoni kabla ya kumwagiza mpigaji aikate kwani alikuwa bize.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours