Mshambuliaji wa Bournemouth, Dominic Solanke amechaguliwa kuwa Mchezaji bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu England.
Solanke ameshinda tuzo hiyo baada ya kuifungia klabu yake hiyo magoli 6 ndani ya mwezi huo.
Solanke (26) alikulia kwenye shule ya vipaji ya Chelsea kati ya mwaka 2014-2017, kabla ya kujiunga na Liverpool na baadae akatimkia Bournemouth mnamo 2019.
+ There are no comments
Add yours