Winga wa Argentina Ángel Di María amethibitisha Alhamisi kwamba maisha yake ya kimataifa yatafikia kikomo baada ya michuano ya Copa América 2024 nchini Marekani.
Mshambulizi wa Argentina Angel Di Maria atastaafu kucheza soka la kimataifa kufuatia Copa America mwaka ujao.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alisema Alhamisi baada ya kuiwakilisha nchi yake kwa miaka 15.
Di Maria amecheza mechi 136 akiwa na mabingwa wa dunia Argentina tangu alipocheza kwa mara ya kwanza mwaka 2008, akicheza katika Kombe la Dunia mara nne na kufunga katika fainali ya 2022 dhidi ya Ufaransa.
Atashiriki michuano yake ya sita ya Copa America kwenye michuano ya Juni 20-Julai 14 nchini Marekani, ambapo Argentina itajinadi kutetea kwa mafanikio taji lao la bara.
Fainali zote alizofunga bao Angel Di Maria Argentina hawajawahi kupoteza.
+ There are no comments
Add yours