Jaji Juan Merchan wa Mahakama kuu ya New York, ameamuru Rais mteule wa Marekani Donald Trump ahukumiwe kabla ya kuapishwa, katika kesi ya kughushi rekodi.
Hata hivyo, Jaji huyo ametoa viashiria kuwa hukumu hiyo haitakuwa ya kifungo.
Mnamo Mei 2024, Trump alikutwa na makosa 34 yaliyohusisha kuficha rekodi ya pesa ambazo Muigizaji Stormy Daniels alilipwa mwaka 2016 wakati wa kampeni ya Trump ili asitoe taarifa za uhusiano waliowahi kuwa nao.
Hukumu hiyo imepangwa kutolewa Januari 10, ikiwa ni siku 10 kabla ya uapisho. Hali hii bado inamuweka Trump kwenye mkondo wa kuwa Rais wa kwanza kuingia madarakani akiwa amekutwa na hatia ya uhalifu.
Msemaji wa Trump, Steven Cheung, amesema kuwa kesi hiyo haizingatii sheria na kuwa Jaji amechanganyikiwa.
+ There are no comments
Add yours