Tetesi za kandanda ni kuwa mchezaji Lionel Messi atajiunga tena na Barcelona baada ya mkataba wake wa sasa na Paris Saint-Germain utakapomalizika 2023.
Messi alijiunga na Barcelona katika ujana wake na alitumia miaka 17 yenye mafanikio makubwa katika kikosi chao cha kwanza. Lakini muda wake Barca ulifikia kikomo mwaka wa 2021. Messi alitaka kuongeza muda wake wa kukaa lakini matatizo ya kifedha ya Barca yalimzuia kufanya hivyo. Alijiunga na PSG kwa mkataba wa miaka miwili na kwa sasa anatamba katika klabu hiyo ya Ufaransa.
Lakini inaonekana muda wake nchini Ufaransa utafikia tamati mwishoni mwa msimu. Hiyo ni kwa sababu mwanahabari wa Argentina Veronica Brunati ameripoti kuwa atajiunga tena na Barca wakati kampeni ya 2022/23 itakapokamilika.
+ There are no comments
Add yours