Mh. Bwire Kuandaa Mashindano Ya Kwaya Taveta

Estimated read time 1 min read

Mbunge wa Taveta Mheshimiwa John Bwire ametangaza Zawadi ya Krismasi Kwa Kwaya zinazofanya Vizuri Kwa Kuwatengea washindi watatu wa Kwanza kitita Cha Shilingi Laki Moja (100K).

Mashindano hayo yataanza wiki ijao katika Kila wadi na washindi wawili Kwa kila wadi watachuana siku ya Jamuhuri, Tarehe 12 Decemba, 2023

Kulingana na ratiba ya mashindano hayo:-

Jumatatu ya Tarehe 27 itakua zamu ya Mboghoni na Kwaya Zote zitakutana Kiwalwa Social Hall.

Jumanne Tarehe 28 ya Mwezi huu Kwaya Za Mahoo zitakua Danida Hall.

Jumatano Wana Mata Watakutana Kimala Social Hall.

Alhamisi itakua Zamu ya Bomeni kuchuana Satoo hall.

Na ijumaa itakuwa siku ya Chala ambapo mashindano hayo yataanza na Chala Chief’s office saa Tatu asubuhi alafu Saa Saba Kamili kufanyika tena Chumvini Polytechnic.

Hakuna malipo ya kujiandikisha .

Kwa Maelezo zaidi wasiliana na Mratibu wa Ofisi ya Mbunge Ndugu Pascal Kipande Mr. Chairman…. 0704024286 / 0758758576.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours