Mtoto Ametelekezwa Katika Kituo Cha Soko Huko Taveta

Estimated read time 1 min read

Mapema Alhamisi asubuhi mtoto mchanga alipatikana akiwa ametelekezwa katika kituo cha Soko la Njukini eneo bunge la Taveta. Mtoto huyo wa kike, ambaye umri wake kamili bado haujafahamika alipatikana kwenye mlango wa duka la mboga asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa katika kituo cha Polisi cha Chumvini Njukini, tukio hilo liliripotiwa na mfanyabiashara ambaye alimpata mtoto huyo.

Polisi wamempeleka mtoto huyo katika kituo cha afya cha Njukini kwa ajili ya dawa na uchunguzi huku uchunguzi kuhusu waliko wazazi hao ukianza. Wenyeji wameombwa kuripoti visa vyovyote vya kupotea kwa watoto au visa vyovyote vya akina mama wachanga kuwatelekeza watoto wao kwa shinikizo kutoka kwa familia zao.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours