Muabori Asema Hana Beef na Msanii Yeyote Awatakia Wasanii Wenzake Kila la Heri Ya Siku ya Wapendanao.

Estimated read time 2 min read

Baada ya Muabori kuchapisha maneno tatanishi yanayo ashiria ako na bifu na msanii fulani kwenye ukurasa wake wa facebook mnamo tarehe 6 February, 2022, msanii huyo amejitokeza tena siku ya Valentine a kueleza kinaga ubaga kuwa hana bifu na msanii yeyote kwani industry ya mziki ni kubwa na kila msanii ako na wafuasi wake.

kwenye ukurasa wake wa facebook mnamo tarehe 6 February, 2022

Msanii huyo kupitia ukuruasa wa facebook tarehe 14 February, aliweza kuchapisha picha za baadhi ya wasanii wa Taveta na maneno ya kuwatakia kila la heri kwenye safari ya mziki

Nikimnukuu

“Leo ni siku ya kuonyesha upendo,na mm kama msanii ni siku yangu ya kuonyesha upendo kwa wasanii wenzangu wa nyumbani.Sina tofauti au #beef na msanii yoyote kutoka Taveta na haitawahi tokea,ndoto yangu ni kuona Taveta ikiwa kisiwa cha #mastar na watu wa maana.#Music_Industry ni pana sana na kila msanii ana nafasi ya kufanikisha ndoto yake,bila kugombana na wenzake.Kulingana na mm beef inaruhusiwa iwapo wasanii wawili,wameamua kukaa chini na wakaamua kufake beef ili kuchangamsha mafans na ku market kazi zao.But sio personal!Naamini Taveta imebarikiwa na vipaji,ila hatuna upendo,umoja na pia mashabiki wanafaa kusupport wasanii hasa wale wako huko home.Hii tabia mashabiki kudharau wasanii eti,msanii gani huna hela,huna gari etc.Ni kutoelewa,msanii anafaa kuwa na kipaji,pesa ni kitu tofauti sana.Kuna tofauti ya #utajiri na #kipaji.Kiufipi: Tunahitaji upendo❤️ baina yetu sisi wasanii na pia upendo ❤️ kutoka kwa mashabiki. Happy Valentines 🌹

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours