Emily Campagno aliwashangaza Wakenya alipotoa madai ya uwongo kwamba katika nchi kama Kenya, wanawake wajawazito hawana haki ya kupiga kura.
Alikuwa akilinganisha Kenya na Marekani.
“…Nchini Kenya ambapo wanawake wajawazito hawawezi kuondoka nyumbani kwa hivyo hawana haki ya kupiga kura,” alisema.
Kauli yake si ya kupotosha tu, bali pia inaonyesha upendeleo alionao dhidi ya Kenya.
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wameitaka Fox News kuondoa video hiyo na mwanahabari huyo kuomba msamaha.
+ There are no comments
Add yours