Mwanahabari wa Mombasa Fatma Rajab, mwenye umri wa miaka 27 amefariki dunia baada ya kuugua. Mwanahabari huyo alikuwa amepelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi cha hospitali ya Coast General Teaching and Referral ICU alikata roho mwendo wa saa sita mchana Jumamosi, siku mbili baada ya juhudi za wanahabari wenzake na MCA wa Kadzanani Fatma Kushe kuhakikisha anapata matibabu bora zaidi.
Fatma, ambaye pia alifanya kazi Radio Salaam kabla ya kuhamia Mo Radio, alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa baridi yabisi, hali ambayo valvu za moyo zimeharibiwa kabisa na homa ya baridi yabisi.
+ There are no comments
Add yours