Mwanamuziki Profesa Jay Alazwa Hospitalini, Familia Yaruhusu Mchango.

Estimated read time 1 min read

Mbunge wa zamani wa Mikumi na msanii wa Hip Hop, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay, amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Taarifa za kuugua kwake zilisambaa katika mitandao na tangazo likiomba kuchangia matibabu ya msanii huyo. Familia ya profesa Jay imethibitisha kuwa Joseph Haule anaumwa na anaendelea kupatiwa Matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na anaendelea vizuri kiasi.

Mkewe wake Profesa Jay amethibitisha kuwa wameruhusu michango hiyo huku akieleza kuwa kwa wiki moja wanatumia Sh4 milioni kwa matibabu yake hivyo wameona watoe nafasi kwa watu wake kumchangia matibab

Familia ya profesa Jay imethibitisha kuwa Joseph Haule anaumwa na anaendelea kupatiwa Matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na anaendelea vizuri kiasi.

Baadhi ya wasanii wameweza kuweka tangazo hilo kwa mitandao wakiomba mashabiki wao na wafuasi wa Profesa Jay kumchangia msanii huyo.

Image
Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours