Ukistaajabu ya Musa basi utayaona ya Firauni kuna mwamamke mmoja ambaye ni mwandishi wa kitabu chenye jina lenye maana sawa na kusema ”Jinsi ya kumuua mume wako” ambaye anatokea Marekani anaetambulika kwa jina la “Nancy Crampton Brophy”, mwenye umri wa miaka 71 amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya mume wake aliyoyatekeleza mwaka 2018.
Kulingana na ripoti imeelezwa kwamba tukio la mauaji lilifanyika mahali ambapo marehemu mume wake alietambulika kama “Daniel Brophy”, alikuwa akifanya kazi kama mpishi na mwili wake ulikutwa sakafuni kwa majeraha ya risasi mbili mnamo Juni 2018.
Nancy Crampton Brophy, amehukumiwa maisha mnamo Juni 13, 2022, na kwamba hata silaha aliyoitumia haijulikani ilipo.
+ There are no comments
Add yours