Bongo movies imepoteza moja ya waigizaji wa mfano aliyekuwa kioo cha jamii kimaadili kwa vitendo kuanzia uvaaji, mahusiano na watu.
Grace Mapunda hakuwa mtu wa skendo mitandaoni, hakuwa mvaaji wa zile nguo za nusu uchi hayo hayakuwa maisha yake
Alichagua kuwa mama mstaarabu wa kawaida kabisa asiye na makando kando
Binafsi sijawahi kusikia skendo yoyote ya kipuuzi Grace Mapunda akitajwa kuhusika, hakika alifanikiwa kujiheshimu na kuzishinda changamoto za umaarufu
+ There are no comments
Add yours