Ni kumbukumbu gani uko nayo ukikumbuka barabara ya Taveta-Voi kabla iekwe lami?

Estimated read time 1 min read

Kama unafahamu ile nyimbo ya “safari ya bamba” basi hiyo ndio ilikuwa hali halisi kwa wasafiri wa Taveta. Safari ya kutoka Taveta kwenda Voi ilikuwa inagharibu masaa nne ama tano kulingana na hali ya anga.

Safari hiyo ilikuwa inakulazimu ufike voi utafute mahali uoge na ubadilishe nguo maana ulikuwa unakaa ni kama umetoka kwa shimo. Ukipatana na mtu wa Taveta mjini Voi ungemtambua kwa urahisi sana kwa kumwangalia kichwa. Tofauti na wachimba migodi ilikuwa mmoja kachafuka bila kupata dhahabu.

Makosa itokee ukose ticket ya basi kubwa kama Tukutendereza na badala usafiri na Nissan.

Wanafunzi wa kutoka Taveta walikuwa wakichekelewa sana wakifika shule. Maana huwezi tofautisha wametoka nyumbani ama wametoka kuchimba visima.

Je ni kumbukumbu gani uko nazo ukikumbuka hiyo barabara? Usikose kutoa maoni yako kwa comment line hapo chini

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours