Mrembo mmoja Taveta amejitwika jukumu na kueleza masaibu wasichana mjini Taveta wanapitia. Kulingana na malalamishi aliyotoa Vijana Taveta wamezembea kazi. Msichana anatoka nyumbani kwao akitembea njiani angalau apatane na kijana amwombe lakini hakuna mwenye anaonyesha bidii. Nikimnukuu.
“Swali tu TVT ilibadilika lini hata nashanga.nikitembea barabarani sipati hata kamwanaume kakinisimamisha n kuniomba number hata wa salamu tu hakuna kama kitambo.sasa nashindwa wanaume ndo wanatuogopa sisi madem au n sisi madem ndo tumekaa mkao wakuto vutia wanaume ama wale mimi hukutana na wao wote wanafamilia zao yani waliowa .tutaishije hivi jamani bila kutongozwa. Na raha ya madem kutogozwa turinge bana alaaaaaaaaaaaaa.kama wote taking mutuambie tuangalie kwengine tusing’oje Embe chini ya mnazi.nipigieni makofi kama nimeongea point”
Swala hilo limegusa wengi kwanza kina dada wengi wakijitokeza kumuunga mkono, ikionekana ni swala limekuwa likiumiza kina dada wengi wa Taveta. Vijana wengine wamejitokeza wakijitetea ni hali ya uchumi imesababisha, wengine wakisema ni tabia za kina dada za kula fare. Wengine wamejitokeza kuomba namba. Je ni kweli vijana wamezembea ama tatizo liko kwa kina dada?
Haya hapa baadhi ya maoni ya watu..
Jiunge na Mjdala huu kwa mtandao wa facebook
+ There are no comments
Add yours