Nimepitia mengi katika siku 462 nilizokaa kitandani, nimeona nimshukuru Mungu kwa ajili ya kipindi chote hicho na kunifanya niendelee kuwa hai hadi sasa na niwashukuru pia Watanzania kwa maombi na michango.
Msanii wa Bongo Flava, Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay asimuliza mateso aliyopitia wakati akiugua. Mwanamziki huyo alieleza mateso ya kukaa ICU siku 462 ambayo anasema haikuwa rahisi na anamshukuru Mungu na mashabiki wake kwa maombi.
Profesa Jay amewachilia wimbo mpya ambao alioupa jina la 462 ambao ni sawia na mwaka mmoja na miezi mitatu zenye alikaa ICU akiugua ugonjwa wa figo.
Profesa Jay ameanza kwa kuandika “Salaam Ndugu zangu, kwanza namshukuru sana MUNGU aliye hai kwa uponyaji na kunipa nafasi nyingine ya kuendelea kuwa hai, hali yangu ilikuwa mbaya isioelezeka, asante sana Mungu baba (nitakutukuza na kukusifu siku zote za maisha yangu), pili kipekee namshukuru sana Mhe. Rais Dr. Samia Hassan Suluhu na Serikali yake kwa kunigharamia matibabu yangu yote ya Muhimbili na Nje ya Nchi, Asante sana Mama pamoja na Serikali yako yote kwani Viongozi wako wa chama na serikali walikuwa wanapishana kila siku kuja kuniona na kunifariji”
Profesa Jay ambaye kwa sasa afya yake inaendelea kuimarika ameachia wimbo mpya unaoelezea maisha aliyopitia katika kipindi hicho cha ugonjwa kuanzia alivyoanza kuumwa hadi kupata nafuu.
Katika wimbo huo aliomshirikisha mwanamuziki wa injili Walter Chilambo, Profesa Jay ameimba akieleza hatua kwa hatua ya ugonjwa wake hadi kulazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi.
+ There are no comments
Add yours