Raila Aikosoa Serikali Ya Ruto Kuhusu Kufukuzwa Kwa Watu 3,000 Mjini Voi.

Estimated read time 1 min read

Kinara wa Azimio Raila Odinga ameikosoa serikali kuhusu kufurushwa kwa watu 3,000 kutoka eneo la Msambweni kaunti ya Taita Taveta iliyotokea mapema Jumamosi asubuhi.

Takriban wakaazi 3000 wa Msambweni eneo bunge la Voi wamekumbana na ubomoaji ambao umewaacha wakilia kwa maumivu makali na kukata tamaa.

Huku akimsuta Rais William Ruto kuhusu kile alichokitaja kuwa kufurushwa kwa nguvu, Waziri Mkuu huyo wa zamani alifichua kuwa alizungumza na viongozi wa Voi katika jitihada za kutafuta suluhu la amani kwa suala hilo.

Kulingana na kiongozi huyo wa upinzani, jamii hiyo hapo awali iliomba serikali kuwafidia ardhi iliyochukuliwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Standard Gauge (SGR) ili kuwawezesha kuishi kwingine lakini maombi hayo yaliangukia kwenye masikio. Ufurushaji huo ulioanza Jumamosi asubuhi ulihusisha kikosi cha maafisa wa polisi waliovamia eneo hilo wakiwa na kikosi cha ubomoaji ambacho hadi sasa kimeangusha nyumba kadhaa kwenye kipande cha ardhi kinachozozaniwa.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours