Kiongozi wa Azimio Raila Odinga ameikashifu serikali kwa kuwataka Wakenya kulipa ili kupata vitambulisho vya Kitaifa au kulipia hata zaidi ikiwa utapoteza kitambulisho.
Raila alisema ni hatia kwa raia kutakiwa kulipia hati zinazoonyesha wao ni Wakenya.
“Mtu anataka ununue kitambulisho ili kuonyesha kuwa wewe ni Mkenya, Unawezaje kuombwa ulipe ilhali baba na mama yako wote ni Wakenya,” Raila aliuliza.
+ There are no comments
Add yours