Raila Odinga ametofautiana na msimamo wa rais wa Kenya William Ruto kuhusu mzozo huo na kumshauri kutosalia kimya dhidi ya dhulma kwa Wapalestina.
Rais William Ruto alikuwa mmoja wa viongozi wa ulimwengu kusimama na Israel kufuatia uvamizi wa Oktoba 7.
“Nikiwa hapa Mombasa, nataka kutoa ushauri kwa bwana Netanyahu, Netanyahu, Netanyahu, wacha kuua watoto wakiarabu wa Palestine,” Raila amesema.
“Lazima tulaani kwa maneno makali iwezekanavyo, ukatili uliokosa ubinadamu ambao watoto na wanawake wasio na hatia, wananyanyaswa na utawala wa Netanyahu. Ni unyama,” Raila Odinga ameongeza.
+ There are no comments
Add yours