Rapa Ye Almarufu Kanye West Apoteza Ubilionea

Estimated read time 2 min read

Kampuni ya mavazi ya Adidas imekata mahusiano yake na rapa Ye, anayejulikana kama Kanye West, na kusema “haivumilii chuki dhidi ya Wayahudi na matamshi yoyote ya chuki”

Jarida la Forbes limesema kitendo cha Rapper Ye (Kanye West) kutoelewana na Washirika wake wa kibiashara kimemgharimu hadhi yake ya kuwa Bilionea, katika wiki za hivi karibuni, jumba la kifahari la Balenciaga, Gap na Adidas walivunja mikataba yao huku wakimaliza uhusiano wa kibiashara na Ye (Kanye West) kwa kujihusisha na maneno ya chuki.

Mapema wiki hii jarida la Forbes ambalo ni moja ya Wafuatiliaji wakubwa wa utajiri wa Watu mashuhuri ulimwenguni lilitangaza kuwa limemtoa Ye kutoka kwenye orodha yake ya Mabilionea, Forbes awali walikadiria kuwa dili la Adidas lilichangia Dola Bilioni 1.5 za thamani yake lakini Forbes sasa inakadiria kuwa utajiri wa Ye unafikia Dola Millioni 400.

Forbes wamesema kiasi cha Dola Milioni 400 zilizosalia kwenye utajiri wake zinatokana na nyumba, pesa taslimu, orodha ya nyimbo zake na asilimia 5 ya hisa katika kampuni ya mavazi ya Mke wake wa zamani Kim Kardashian, Skims.

Bila shaka, kuna uwezekano kwamba Ye bado anajiona kama ni Bilionea, ikizingatiwa kwamba amekuwa akilalamika kwa miaka mingi kwamba Forbes ilikuwa ikidharau thamani yake.

Itakumbukwa Forbes iliripoti mwaka 2020 kwa mara ya kwanza kwamba Kanye amefikia hadhi ya Bilionea na Kanye alituma ujumbe kwenye jarida akisema “Sio Bilioni 1, ni Dola Bilioni 3.3 kwani hakuna Mtu wa Forbes anayejua kuhesabu”

Nukuu: Millard Ayo

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours