Timu ya Green boys kutoka maeneo ya Mwananyamala leo alasiri imeweza kuichakaza Kwale United kutoka Kwale mjini baada ya kuitandika mabao 3 -1 bila huruma kwenye mechi ya kuwania kufuzu kwa Robo fainali ilio garagazwa kwenye uga wa shule ya msingi ya Waa.
Green boys walijipata chini pale Kwale United walipo tangulia kucheka na wavu mwanzoni mwa kipindi cha kwanza lakini hawakufa moyo.
Kipindi cha pili kilipo anza Green boys walipandisha mori na kufanya mashambulizi makali kwenye lango la wapinzani wao mpaka wakasawazisha bao walilo kuwa wamefungwa.
Baada ya kusawazisha vijana hawo wepesi walituliza boli na kuanza kuwa angaisha wapinzani wao mpaka wakapata bao la pili na la tatu.
Captain wa Kwale United alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kadi za njano mbili na kutolewa nje ya mchezo kwa kupinga mahamuzi ya rifa mwisho mwisho mwa kipindi cha pili.
Green boys sasa watakuwa ni wenye kupimana nguvu na Vivah Manyota kwenye michuano ya robo fainali.
+ There are no comments
Add yours