RHYNO : HATUWEZI KUTAJA UGONJWA UNAOMSUMBUA PROFESA JAY NI JAMBO LA FARAGHA

Estimated read time 1 min read

Black Rhyno ambaye ni Msemaji wa Familia ya Profesa Jay amesema hawawezi kutaja ugonjwa unaomsumbua Profesa Jay kama wengi wanavyotamani kufahamu kwani ugonjwa ni jambo la faragha.

“Kuhusu Prof. Jay anaugua nini, maradhi ni privacy ya Mgonjwa na tunaheshimu privacy yake kwa sasa hivi tuheshimu privacy yake hatuwezi kuzungumzia maradhi ya Mtu tunakuwa tunakiuka utu na ethics za mgonjwa, siku akiimarika kabisa akiamua kusema alikuwa anaumwa nini ni sawa lakini kwa sasa tuache kama ilivyo”

“Yupo sehemu salama kwa sasa baada ya kutoka Hospitali ila muda ambao atachukua hapo hatuwezi kusema ni mambo ya Mungu ni mengi, tunaweza kusema miezi akakaa wiki moja akawa ameshapona kwa sasa yupo sehemu salama, afya yake ipo sawa anaendelea tu na mazoezi ya viungo, lishe n.k, zaidi akiwa tayari ameimarika mtasikia”

Kupitia nukuu ya : Millard Ayo

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours