Baada ya Nay wa Mitego kudai kwamba wimbo wake mpya wa “Amkeni” ambao umezua gumzo baada ya kuleta utata kwamba aliyemtumia wimbo huo ni Roma Mkatoliki. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Roma amekanusha tuhuma hizo, ambapo ameandika
“YAH: SUHUSIKI KWENYE HILI
Kwenu Basata Tanzania, husika na kichwa cha Habari hapo juu, huyu kijana NAY ni muongo sana, mimi sijamtuma kitu chochote wala sijahusika kwenye wimbo wake huo, kwanza hata namba yake ya simu sina, ananisingizia na sijapenda, mimi ni kijana muadilifu sana na mnalijua hilo toka kuzaliwa kwangu, Basata Tanzania”
“Naipenda sana nchi yangu, zidumu fikra za Mwenyekiti na kazi iendelee
Akija huyo Jumatatu malizaneni naye peke yake, mimi nina familia na watoto wananitegemea kupitia huu mziki sitaki HEKAHEKA saizi!!
Kwanza mimi urafiki na mtu FREEMASON wapi na wapi jamani, Basata Tanzania hata nyie hamuoni!!”- ameandika Roma.
+ There are no comments
Add yours