Safaricom Yazindua Tawi Addis Ababa, Ethiopia

Estimated read time 2 min read

Safaricom leo, Oktoba 6, imezindua mtandao wake wa Ethiopia unaoanza kufanya kazi katika miji 11. Katika hafla iliyohudhuriwa na Rais William Ruto mjini Addis Ababa,

Safaricom Ethiopia ilianzisha mtandao na huduma zake za mawasiliano ya simu katika mikoa 11. kuanzia leo wenyeji wa mikoa hiyo watafikia huduma za 2G, 3G, na 4G za Safaricom huku mipango ya kupanuka hadi miji mingine 25 ifikapo Aprili 7, 2023, ikiendelea.

Safari ya kutambulisha huduma nchini Ethiopia imekuwa ndefu. Baada ya zabuni nyingi na kuidhinishwa na serikali, Safaricom ilipewa idhini ya kuanza kufanya kazi nchini Ethiopia mwaka jana. Mkurugenzi Mtendaji wa Safaricom Group, Paul Ndegwa katika taarifa alisema anaamini kampuni hiyo itatumia uzoefu wa miaka mingi kubadilisha sekta ya mawasiliano ya Ethiopia.

“Tunatazamia kuwa na matokeo chanya kwa watu wa Ethiopia kwa mtandao endelevu na bora wa simu ambao utakuwa njia muhimu ya kuzindua huduma za mawasiliano ya kidijitali nchini kote kwa zaidi ya Waethiopia milioni 118.”

Wakati akipongeza uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone Group Nick Read alisema, “Tunafuraha kuwa sehemu ya muungano huu wa kimataifa wenye uzoefu mkubwa, wenye maono thabiti ya kuendeleza jumuiya ya kidijitali ya Ethiopia, yenye malengo ya wazi ya kutoa matarajio makubwa zaidi ya elimu, kazi, na ustawi.”

Safaricom Ethiopia ni kampuni tanzu ya kampuni kubwa zaidi ya mawasiliano ya simu ya Kenya na ambayo itakuwa uwekezaji wa kwanza wa kigeni katika eneo la mawasiliano ya Ethiopia. Serikali ya Kenya ina asilimia 35 ya hisa katika Safaricom.

Raisi William Samoei Ruto, katika safari yake Ethiopia analenga kuboeresha miundo misingi kwa nyanja mpya katika mahusiano ya Kenya na Ethiopia ili kufuata maslahi ya pamoja, hasa katika eneo la teknolojia, kwa ustawi wetu wa pande zote.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours