Mfanyabiashara, Mtayarishaji wa muziki ambaye ni CEO wa Lebo ya Mavins kutoka Nchini Nigeria @donjazzy amemsaidia Shabiki aliemuomba Msaada kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Shabiki huyo alimuandikia ujumbe kwenye comment akisema kuwa yeye na Familia yake wanapitia magumu kwani wanaishi kwenye kibanda kiasi kwamba hali ya baridi kali usiku wa manane inamuathiri mtoto wake yote ni ukosefu wa fedha.
Shabiki huyo alimuomba Don Jazzy kiwango cha laki mbili na nusu pesa ya Kenya ili aweze kufungua tovuti ambayo ataweza kuendeleza biashara yake na kuimudu familia yake.
Sasa baada ya ujumbe Kupitia twitter DonJazzy amethibitisha kumtumia Shabiki huyo kiasi cha Milioni 5 ili imsaidie kujikimu na Familia yake.
+ There are no comments
Add yours