Sherehe mjini Damascus huku wapinzani wa Syria wakitangaza kumalizika kwa utawala wa Bashar al-Assad.

Estimated read time 1 min read

Aliyekuwa Rais wa Syria, Bashar al-Assad ameng’olewa madarakani usiku wa kuamkia leo Jumapili, Desemba 8, 2024, baada ya waasi kuingia katika mji wa Damascus.

Taarifa zinasema Rais Assad na familia yake ambao wameitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 53 wamekimbia kusikojulikana.

Picha za video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha mamia wakivunja sanamu za familia ya Assad ziliopo mjini Damascus.

Milio ya risasi imesikika katika mji mkuu wa Damascus, wakati waasi nchini humo wakiendelea kupambana na vikosi vilivyokuwa vikimuunga mkono Rais Assad.

Rais Assad amekuwa Rais wa Syria tangu mwaka 2000 akipokea kijiti hicho kutoka kwa baba yake aliyefariki dunia Juni 10, 2000.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours