Wizara ya Utalii nchini ipo katika harakati za kubaini vivutio zaidi na mbinu mbadala za kuvutia watalii ili kupiga jeki sekta hiyo kote nchini .
Waziri wa utalii Alfred Mutua ameyasema haya katika kikao na wanahabari kilichofanyika kwa afisi ya gavana wa kaunti hio Andrew Mwadime iliyoko kaunti ndogo ya Mwatate.
Waziri ametaja umuhimu wa kubuni mbinu mpya za kuvutia watalii akisema taifa hili limejikita zaidi katika Utalii wa wanyamapori tangu ukoloni , jambo anasema linafaa kubadilishwa.
Waziri Mutua pia amewakikishia wakaazi kuwa wameweka mipango kabambe ili kufufua sekta ya utalii. Amempa jukumu gavana mwadime achague mahali ili mradi huo uweze kuanza. Mradi huo unapokamilika basi kutakuwa ni soko ambapo bidhaa za utamaduni zitakuwa vinauza kwa watalii wanapozuru kaunti hio.
Vile vile waziri huyo amesema kuwa katika kuajiri makurutu wa shirika la wanyama wa pori jamii zinazopakana na mbuga za wanyama watapatiwa idadi kubwa ililinganishwa na jamii zingine kwani tayari wameshatengeneza mswada huo na hivi karibuni utapelekwa bungeni kujadiliwa. Kulingana na waziri mutua wezi huu wa nne serikali kuu itazindua mfumo mpya wa kutoa fidia kwa watu walioathirika na uvamizi wa wanyama wa pori.
Wakati uo huo gavana Mwadime ameitaja hatua ya wizara hiyo kuahidi kuanzisha sehemu za kuonyesha utamaduni ambapo watalii watalazimika kupitia kujionea urithi huo kuwa itasaidia kuleta motisha kwa wenyeji na kurejesha utamaduni wa jamii ya Wataita na Wataveta.
+ There are no comments
Add yours