Timu ya Tanzania, Taifa Stars, imeonyesha ubabe kwa kuichapa nyumbani timu ya Niger bao 1 – 0 katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.
Bao pekee la ugenini la mchezo huo limefungwa na Charles M’mombwa katika dakika ya 60 ya mchezo.
Ushindi huu unaifanya Taifa Stars kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi E, nyuma ya Zambia, na kuimarisha matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.
Mchezo ujao wa Taifa Stars utakuwa nyumbani, wakipambana na Morocco kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa mnamo Novemba 21, 2023.
Morocco haijacheza mchezo wake kutokana na timu ya Taifa ya Eritrea ambapo pia walikuwa kundi E, kujiondoa.
+ There are no comments
Add yours