Zaidi Ya Wahudumu Wa Bodaboda 100 Eneo La Marungu Kufaidi Mafunzo Ya Udereva

Estimated read time 2 min read

Zaidi Ya Wahudumu Wa Bodaboda 100 eneo la Marungu, kauti ya TaitaTaveta, Kufaidi Baada Automobile Association of Kenya almaarufu AA kwa ufadhili wa shirika la Wildlife Works East AfricaKasigau REDD+ Carbon na Elephant Cooperation kutoa mafuzo kuhusu sheria za barabara na kuendesha magari.

Akiongoza hafla hiyo, Governor Andrew Mwadime – Wakujaa amewataka madereva kuzingatia sheria zote za trafiki, hatua ambayo amesema ndio kinga kamili kwa ajali ambazo zinashuhudiwa si kwa Kaunti pekee bali kote nchini.

Akiongea kwenye kikao na Zaidi ya wahudumu wa bodaboda 100 kutoka wadi ya Marungu, ambao wameanza kupokea mafunzo kuhusu sheria za barabarani na kuendesha magari, yanayotolewa na Automobile Association of Kenya almaarufu AA kwa ufadhili wa shirika la Wildlife Works East AfricaKasigau REDD+ Carbon na Elephant Cooperation, Wakujaa amesema; “Nawarai mtilie maanani mafunzo haya kwani yatawasaidia pakubwa kukabiliana na changamoto mbalimbali ambazo kama madereva mtakumbana nazo barabarani”.

Aidha ametoa wito kwa idara ya trafiki kushirikiana na wanabodaboda ili kuimarisha uhusiano bora miongoni mwao, huku akieleza umuhimu wa idara kuwa vikao vya mara kwa mara wanabodaboda na kuwaeleza kwa kina umuhimu wa kufuata sheria.

Kwa upande wake OCS katika kituo cha polisi cha Maungu Abdi Ali amewataka wanabodaboda kushirikiana na idara ya polisi katika kila hatua akiwataka ambao bodaboda zao zinazozuiliwa katika kituo cha Maungu kuwasilisha stakabadhi muhimu za utambulisho ili waweze kuzipokea.

“Shida kubwa na wahudumu kwenye sekta hii ni ukiukaji wa sheria.nawasihi mnapomaliza mafunzo haya mbadilike na kufuata sheria zote “.

Msimamizi mradi wa REDD + eneo la Kasigau Nick Taylor amempongeza serikali ya kaunti chini ya gavana Mwadime kwa ushirikiano na bidii ya kuhakikisha wananchi wanazidi kuona faidi ya utunzaji mazingira kupitia uuzaji wa hewa kaa (Carbon Credit).

Maafisa wa utawala wakiongozwa na ACC wa divisheni ya Nyangala Agnes Wangare,mwakilishi wa wadi Stephen Mkala, waziri wa vijana, michezo, jinsia na utamaduni Shedrack Mutungi, mshauri wa kisiasa wa gavana Richard Lukindo, naibu mkurugenzi wa mawasiliano Harrison Kamwana, ni miongoni mwa waliokuwa katika hafla hiyo.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours