Toleo la 8 la Tuzo la ‘All Africa Music Awards’ AFRIMMA lilifanyika Dakar, nchini Senegal,huku ikishuhudia baadhi ya wasanii mashuhuri zaidi barani Afrika wakipewa sifa na kusherehekewa kwa bidii na ustadi wao katika kazi zao.
Watu mashuhuri kutoka mabara mbalimbali walialikwa kwenye hafla hiyo ya kuwapongeza wasanii bora wa muziki barani Afrika kwa mwaka 2023. Upande wa Afrika mashariki tuzo hizo zimeenda kwa wasanii kama vile Diamond Platnumz ameibuka mshindi wa Tuzo ya msanii bora Afrika mashariki pia Nadia Mukami akiibuka msanii bora wa Kike Afrika Mashariki.
Baadhi ya Wasanii wengine walioibuka na Tuzoni pamoja na the Late AKA ‘Best male’ southern Africa huku Nadai Akai akiwa msanii bora kike Afrika kusini, Ayra Starr nae akiwa amechukua msanii bora wa kike Afrika Magharibi pamoja na Davido akiwa amechukua Albamu bora ya mwaka.
+ There are no comments
Add yours