Utafanya nini ikipata Benki imekuwekea pesa zisizo zako kwenye account? utazichomoa fasta au utawaambia Benki waache kukutafutia dhambi? Ama utaenda kwa shirika la upelelezi ili usijipate kwa kashfa za ufujaji wa pesa?
Huko Marekani, Benki moja ilikosea na kuweka Dola za Kimarekani BILIONI 50 kwenye account ya familia ya Jamaa mmoja na kuziacha pesa hizo kwa siku nne.
Benki ilikiri kutokea kwa hitilafu hiyo na kuziondoa pesa hizo huku Jamaa huyo akisema baada ya kuona pesa hizo yeye na Mke wake hawakushawishika hata kidogo kutumia hata dolla moja “hatuwezi kuigusa hiyo pesa, sio yangu, sio ya jasho langu”
+ There are no comments
Add yours