Vijana wa Mombasa kufaidi katika mpango wa kuhakikisha usalama wa ufuo na mtiririko wa trafiki

Estimated read time 1 min read

Zaidi ya vijana 2,000 kutoka kaunti ya Mombasa watapata watafaidi kupitia ajira na mafunzo ya ujuzi kupitia mpango wa ‘Mombasa Yetu Programme’ uliozinduliwa Alhamisi na Gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir na viongozi wengine waliochaguliwa kutoka kaunti hiyo.

Mpango huo utashuhudia vijana wakifanya kazi ya usafi na urembo, usalama na mtiririko wa trafiki katika kaunti ya Mombasa.

Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir pia aliongezea kuwa vijana hao watapewa nafasi ya kufanya kazi na kuwa na uzoefu katika sekta ya utalii ndani ya kaunti hiyo.

Ilikuwa furaha yangu kuzindua mpango wa Mombasa Yetu ambao utatoa ajira kwa njia ya mafunzo ya ujuzi kwa vijana 2,000 mjini Mombasa. Mpango huu utakuwa na vijana hawa watashughulika na usafi na urembo, usalama na mtiririko wa trafiki pamoja na uboreshaji wa uzoefu wa utalii katika Kaunti ya Mombasa. Vijana hawa pia watafanya kazi kuzunguka fukwe zetu ili kutekeleza utiifu wa sheria zilizowekwa na mamlaka ili kuhakikisha kuwa hatuna ukiukwaji wa usalama karibu na fukwe zetu. Wale walioajiriwa katika mpango huu watalipwa kila wiki. Kama Gavana wako Mtumishi, nitahakikisha wafanyakazi wanatendewa kwa heshima na malipo yao yanafanyika kwa wakati” Alisema gavana wa Mombasa Abdulswamad Nassir

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours