Vinicius Junior ‘Vini Jr’ anastahili kushinda tuzo la ‘Ballon d’or’ 2024 – Karim Benzema

Estimated read time 1 min read

MCHEZAJI wa zamani wa Real Madrid Karim Benzema, amesema nyota wa timu ya taifa ya Brazili na Real Madrid Vinicius Junior ‘Vini Jr’ anastahili kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2024 ‘Ballon d’or’ inayotolewa na gazeti la Ufaransa.

Kupitia Marca Benzema alisema Vini Jr alikuwa na msimu mzuri na Mabingwa hao wa Ulaya na Hispania.

“Ninaweza kusema Vini Jr anastahili kubeb tuzo ya Ballon d’or kwa mwaka huu, kwa sababu amekuwa na mchango mkubwa katika timu yake,” amesema Benzema.

Msimu wa 2023/24 katika Ligi Kuu ya Hispania Vini Jr alifunga mabao 15 katika mechi 26 na akiwa amefunga mabao sita na kupiga pasi nne za mabao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Benzema ambaye anacheza katika timu ya Al Ittihad ya Saudia Arabia aliwahi kushinda tuzo ya Ballon d’or mwaka 2022 baada ya kuisaidia Real Madrid kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu nchini Hispania.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours