Viongozi Wanaomuunga Mkono Kalonzo Wapuzilia Mbali Njama Ya Kupindua Siasa Za Ukambani

Estimated read time 1 min read

“Mheshimiwa Stephen Kalonzo Musyoka anasalia kuwa kigogo wa siasa na msemaji wa eneo la Ukambani. Kwa hivyo, tungependa kuwaambia watu wanaotoa madai hayo kua wanaota mchana,” seneta Mutula aliyasema hayo kwenye kikao na wanahabari katika makao makuu ya Wiper, Karen, mjini Nairobi.

Magavana watatu wa ukambani, Alfred Mutua (Machakos), Charity Ngilu (Kitui) na Profesa Kivutha Kibwana, Jumatano asubuhi walifanya mkutano mjini Machakos. Mkutano huo unasemekana unahusu siasa za urithi wa uchaguzi mkuu mwaka huu. Walitarajiwa kutoa taarifa kuhusu siasa za urithi wa urais.

Wakati huo huo, wandani hao wa Bw Musyoka walisema chama cha Wiper kiko imara na hakina wasiwasi wowote kuhusiana na madai kuwa vyama vya ANC na Ford Kenya vinapanga kufanya kazi na mrengo wa Naibu Rais William Ruto.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours