Wabunge Waidhinisha Hoja Ya Kumbandua Waziri Wa Kilimo Mithika Linturi

Mnamo Alhamisi, Mei 2, wabunge 149 walipiga kura kuendelea na mchakato wa kumtimua CS Linturi huku 36 kati yao wakiupinga. Ni 3 tu ambao hawakushiriki.

Ili hoja hiyo iendelee, ilihitaji kuungwa mkono na angalau theluthi moja ya wajumbe wa Bunge hilo, jumla ya wajumbe 117. Hii sasa inafungua njia ya kuundwa kwa kamati ya uchunguzi ya wanachama 11.

Muundo wa kamati teule unaonyesha usawa wa uwakilishi bungeni, na nafasi 6 zimetolewa kwa Muungano wa Kenya Kwanza, 4 kwa Muungano wa Azimio la Umoja, na 1 kwa Jubilee Party.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours