Wafanyakazi wa Sauti ya Amerika (VOA) walipokea barua pepe Jumamosi ikiwaweka kwenye likizo ya kulipwa hadi pale watakapoarifiwa na kuwaagiza wasiingie katika ofisi za VOA.
Wakati huo huo, Radio Free Europe/Radio Liberty na Radio Free Asia, ambazo pia zinafadhiliwa na serikali ya Marekani, zimeshuhudia ufadhili wao ukipunguzwa.
Trump na mshirika wake wa karibu, Bilionea Elon Musk, wamekuwa wakijaribu kupunguza ufadhili kwa mashirika na programu nyingi.
Hata hivyo, upunguzaji wa hivi punde ulioelekezwa kwa vyombo vya habari vinavyofadhiliwa na Marekani, unakuja siku moja tu baada ya Trump kuvilaumu hadharani vyombo vya habari vya Marekani kuwa ni vifisadi na visivyo halali.
Wakati wa muhula wake wa kwanza, Donald Trump aligombana na VOA na kuwalazimisha wakurugenzi wake wakuu wawili kujiuzulu mnamo 2020.
+ There are no comments
Add yours