Maelfu ya wakenya mnamo siku ya Alhamisi, Juni 20 waliendelea kukusanyika kufanya maadamano ya amani dhidi ya kupinga mswada wa fedha wa mwaka wa 2024.
Maandamano hayo yaliendelea kwa siku ya pili wiki hii, wakitaka utawala wa Rais William Ruto kuondoa Mswada tata wa Fedha wa 2024.
Mswada huo unalenga kupata mapato ya ziada ya Ksh348 bilioni kupitia nyongeza ya ushuru katika sekta mbalimbali, zikiwemo Ushuru wa Urekebishaji wa Barabara na Ushuru wa Mauzo ya Nje. Maandamano hayo yameenea nchini huku maandamano yakiripotiwa mjini Nairobi, Eldoret, Kisii, Mombasa, Nyeri, Nakuru na Kisumu.
Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) ilitupilia mbali madai kwamba Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome aliidhinisha maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika Alhamisi katika Kaunti ya Nairobi.
Kujibu barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, NPS iliripoti barua hiyo kama bandia.
+ There are no comments
Add yours