Wanajeshi wameungana na polisi kushika doria katika mitaa ya Nairobi huku waandamanaji wa kupinga Mswada wa Fedha wakirandaranda mitaani kuendelea kukaidi Mswada huo ambao tayari umerudishwa Bungeni kwa maboresho.
Kulikuwa na uwepo mkubwa wa maafisa wa kijeshi katika magari ya kivita na ambao walihakikisha waandamanaji hawavunji amani.
Wakati fulani, waandamanaji waliokuwa na furaha waliwashangilia maafisa wa kijeshi walipokuwa wakipiga doria kuzunguka jiji hilo kabla ya kutawanywa na polisi.
+ There are no comments
Add yours