Wavumbuzi wa miundo ya kiuchumi ya “Bottom UP” wakutana hatimaye

Estimated read time 1 min read

Rais William Samoei Ruto hatimaye alipatana na Raisi wa Marekani Joe Biden, kwenye tafrija iliyoandaliwa na Biden wakati wa Kikao cha 77 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York.

Viongozi hao wawili wanapigia debe mfumo wa uchumi wa “Bottom UP” wenye umeleta msisimuko kwa wengi ukimwezesha Raisi William Ruto kushinda uchaguzi wa uraisi nchini Kenya.

Kulingana na maraisi hao wawili wamekuwa wakipigia debe mfumo huo wakisema kwamba mfumo wa uchumi wenye umekuwa ukitumika wa “Trickle Down” hajafaidi wanaichi na ni wakati wa kujenga uchumi wa nchi kuanzia chini kwenda juu.

Rais wa Marekani Joe Biden alielezea nia yake ya kufanya kazi kwa karibu na Rais wa Kenya William Ruto ili kufikia mustakabali mzuri zaidi na salama kwa Wakenya na kwa ushirikiano thabiti kati ya Marekani na Kenya.

Raisi William Ruto aliandamana na mkewe Rachael Ruto kwenye hafla hiyo

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours