Mapozi ni wimbo wa Mr Blue ambao ulitoka miaka 16 iliyopita, chini ya kiwanda cha G.Records zilipozalishwa hit kibao.
Wakali wa tatu, Mr. Blue, Diamond Platnumz na Jay Melody wamekuja pamoja kwenye ngoma moja iliyopewa jina la MAPOZ
Lakini hapa umiliki unakwenda kwa Diamond Platnumz akimshirikisha Mr Blue na Jay Melody ubishi ni mkubwa mtaani kwa sasa ni kuhusu verse ya nani ndiyo imefunika zaidi kati ya Diamond Platnumz, Nyani mzee ‘’Mr Blue’’ na Jay wa Melody.
Wengi wamemsifia Diamond na J Melody kwenye wimbo huu wa Mapoz Ila ni wachache wameuona Unyama wa Mr Blue. Kitendo cha Mkongwe Mr Blue kuingia na ku fit vizuri kwenye Muziki huu ambao una flow za kisasa sio Jambo dogo. Mr Blue amedhihirisha Ukongwe wake kwenye Game
+ There are no comments
Add yours